Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John amefanya ziara ya kukagua jengo la upasuaji (Theatre) linalojengwa katika kituo cha afya cha mishamo na nyumba mbili za watumishi wa afya zinazofanyiwa ukarabati katika kituo hicho.
Baada ya kutoka kituo cha afya cha Mishamo, msafara wa Mkurugenzi Mtendaji ulielekea katika shule ya sekondari Mishamo ambapo alipata fursa ya kuongea na wanafunzi na kuwaonesha njia sahihi ya kuwafikisha na kutimiza ndoto za kuitwa wasomi. Mkurugenzi Mtendaji aliwahamasisha wanafunzi kusoma sana kwa kuanza na kuwauliza maswali (chemsha bongo) na kutoa zawadi za papo kwa papo kwa waliojibu maswali vizuri.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji alitumia muda mwingi kuzungumza na walimu wa sekondari ya Mishamo. Walimu waliwasilisha matatizo yanayokwamisha maendeleo mazuri ya elimu kwa wanafunzi, huku Mkurugenzi akiahidi kuyatatua baadhi ya changamoto.
Sehemu zingine alizotembelea wakati wa ziara ni pamoja na shule ya sekondari Mazwe ambapo alikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa, shule ya msingi Mazwe alikagua pia vyumba vya madarasa vinavyojegwa.
Katika kata ya Ilangu, Mkurugenzi Mtendaji alifika katika shule ya msingi Ilangu, Isuubangala, Mgansa na eneo linalojengwa zahanati katika kijiji cha Kabanga. Wakati katika kata ya Bulamata alitembelea nyumba ya mganga, zahanati na shule ya msingi Bulamata. Pia alifika kujionea ujenzi wa sekondari Bulamata, zahanati ya Busongola, ujenzi wa zahanati ya Kusi na zahanati ya Kamjela.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.