Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Ndugu Albert Msovela amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha kubwa la Samia Day la kutangaza Mafanikio ya Serikali yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 5 ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tamasha hilo litafanyika viwanja vya Shule ya Msingi Inyonga vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, tarehe 04-05/07/2025, na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko.
Lengo ni kumpongeza na kumshukuru Mhe, Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu kwa mchango wake wa kuleta fedha nyingi (Tshs. 1,345,153,585,254.20 Trilioni 1.3) ambazo zimesaidia kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo Mkoani Katavi katika Sekta zote za maendeleo na huduma kwa Jamii.
Tamasha hilo litaenda sambamba na kutembelea hifadhi ya taifa ya Katavi, kutembelea miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Maji wa Miji 28 uliopo Shanwe, Vihenge vya kuhifadhia mazao, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kituo cha kupozea umeme wa Grid ya Taifa.
Aidha RAS-Msovela amewaomba wananchi wote wa Katavi na makundi yote katika Jamii wakiwemo Bodaboda, Wasanii, Bajaji, Mama Lishe, Machinga na makundi mengine kujitokeza kwa wingi katika Matembezi ya Hiari na maadhimisho yote kwa ujumla.
Vilevile, ameziomba Taasisi zote za Serikali na zisizo za Serikali, Mashirika ya Kiraia, Sekta binafsi, Viongozi na Wananchi wa Mikoa ya Jirani na wadau wa maendeleo kujumuika nasi katika tamasha hili kubwa.
KAULI MBIU: “Asante Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za Maendeleo, Katavi Imara na Maendeleo Imara”.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.