Ikiwa umebaki mwezi mmoja tu Mwenge wa Uhuru kupiga hodi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, ukanda wa Mishamo wenye kata 4, na vijiji 16 wameungana na kuweka mikakati madhubuti ya kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Kigoma.
Utayari huo umebainishwa kwenye kikao kazi cha kuhamasisha ushiriki wa wananchi wote katika tukio hilo kubwa kabisa la kitaifa, ambapo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe Onesmo Buswelu, Afisa Tarafa wa Kabungu Bw Alison Uiso amekuwa mgeni rasmi, akiambatana na Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw. Otman Kasamya.
Aidha Bw Uiso ameagiza kufanyika kwa usafi maeneo yote, hamasa iongezeke na amesisitiza ushirikishwaji wa wananchi wote katika maandalizi ya mapokezi ili kutimiza dhana ya umoja na mshikamano.
Katika kikao hicho kilichoambatana na usomaji wa makadirio ya bajeti na michango, Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Bw Otman amewataka wananchi wa ukanda wa mishamo kujitokeza kwa wingi kushiriki mkesha na mapokezi ya Mwenge wa Uhuru na pia amesisitiza suala la sare za Mwenge wa Uhuru kuendelea kusambazwa kila maeneo ndani ya Halmshauri.
Mwenge wa Uhuru utapokelewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Septemba 23.
“Jitokeze Kushiriki Uchaguzi wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.