Timu ya Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ikiongozwa na Afisa Rasilimali watu na Utawala Ndugu Clavery Reginald, aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bw. Shaban J. Juma, imefanya ziara ya siku tatu kwa ukanda wa Mwese na Ukanda wa Ziwa.
Ziara hiyo ya Wataalam imefanikiwa kutembelea zaidi ya miradi 106 ambayo inaendelea kutekelezwa katika maeneotofauti ya Halmashauri.Bw Clavery amesema kwamba lengo kuu la ziara hiyo, ni kuzitatua changamoto mbalimbali zinazofanya miradi baadhi ishindwe kukamilika kwa wakati mpaka sasa licha ya kuwepo kwa pesa za kutosha.
Aidha ameagiza ujenzi wa majengo ya mama na mtoto katika kituo cha afya Ikola uendelee na kuhusu mchakato wa uchunguzi utaendelea kwa wakati uliopita, na kwa sasa kamati zilizoundwa ziendelee na ujenzi huo kwani tayari kuna vifaa vya ujenzi na pesa ya uendelezaji wa mradi ipo.
Sambamba na maagizo hayo, amewapongeza wasimamizi wa miradi hiyo kwa kusimamia miradi vizuri ambapo baadhi ya miradi imekamilika ikiwemo miradi ya matundu ya vyoo na vyumba vya madarasa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.