Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe Onesmo Buswelu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliyetarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya utoaji wa hundi ya mikopo yenye thamani ya Tsh Milioni 525, kwa vikundi vya vijana, wanawake na wenye ulemavu, ameagiza Halmashauri kuwapatia elimu ya kitaalamu wanufaika wa mikopo hiyo ili waweze kujikwamua kimaisha.
Akizungumza katika hafla hiyo DC Buswelu amesema kuwa wanufaika hao licha ya kupata fedha hizo, wengi wao wanakosa elimu na ujuzi wa kuendeleza na kuzalisha fedha hizo, ili waweze kulipa marejesho yao kwa wakati.
Aliongeza kuwa Halmashauri ina fursa nyingi sana ambazo vijana, wanawake na wenye ulemavu wanaweza kufanya biashara, hivyo kama Serikali inapaswa kuwalisha fursa hizo wanufaika na sio kuzificha na kutowapatia kabisa, Halmashauri inatakiwa kuvilea vikundi hivyo ii viweze kukua.
Kwa upande wa Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Halima Kitumba amesema kuwa, wametoa mikopo hiyo kwa vikundi 106 na hivyo wanampango kabambe wa kuhakikisha wanufaika hao wanarejesha fedha hizo kwa wakati.
“Changamoto kwa wanufaika wa mikopo hii wengi wao wanashindwa kurejesha mikopo yao kwa wakati, lakini tunamshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu kuweka utaratibu mzuri wa utolewaji wa mikopo hii, ambapo kuna timu zimeandaliwa mahususi kuanzia Halmashauri, Wilaya na Katani, mikakati tuliyoiweka ili watu kurejesha mikopo kuna kamati za ufuatiliaji zina majukumu yao.”
“Hii ni awamu ya pili kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kutoa mikopo hii, na urejeshaji wa mikopo iko vizuri” Halima Kitumba-DCDO.
Kwa upande wa wanufaika wa mkopo huu, wamemshukuru Mhe Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu kwa kurudisha utoaji wa mikopo hii, na wameahidi kuisimamia kwenye biashara zao ili waweze kurejesha fedha hizo katika Halmashauri kwa wakati ili na wengine waweze kukopeshwa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.