• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Tanganyika District Council
Tanganyika District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanganyika District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

MIGOGORO INACHELEWESHA MAENDELEO - DC BUSWELU

Posted on: January 22nd, 2023

MIGOGORO INACHELEWASHA MAENDELEO - DC BUSWELU.


Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Onesmo Buswelu ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule ili hapo baadae Taifa liweze kupata Mahakimu na Majaji wa kutosha.


Ametoa wito huo wakati akizindua wiki ya sheria kiwilaya leo Januari 22,2023 alipokuwa akihutubia Wananchi waliojitokeza eneo la viwanja vya Shule ya Msingi Mpanda Ndogo Kijiji cha Majalila Kata ya Tongwe.


Pia DC Buswelu ametoa wito kwa Mahakimu na watoa huduma wote katika wiki ya sheria maeneo mbalimbali wilayani humo kutumia nafasi hiyo kuwaelimisha wananchi umuhimu wa elimu na kuwakumbusha kuwa mtoto kupata elimu ni takwa la kisheria.


Aidha, amehimiza Wananchi kutumia fursa hii ya wiki ya sheria kujitokeza kueleza changamoto zinazowakabili badala ya kukaa na migogoro bila suluhu hali ambayo inaweza kupelekea kujichukulia sheria mkononi.


"Migogoro inachelewesha maendeleo, nitoe wito kwa wananchi, Mkisikia matangazo haya jitokezeni njooni mpate elimu bure hamtalipia kwa sababu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anatoa mishahara, anatoa uwezeshaji ili (Mahakimu) waweze kuwafikia. NJOONI MPATE ELIMU HII BURE"


Kwa upande wake Glory Mwakihaba, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi amesema moja ya changamoto walizobaini ni pamoja na wananchi walio wengi kutopenda njia ya usuluhishi  kwa kuamini kuwa kazi ya mahakama ni moja tu ya kufunga watu gerezani.


Amesema kupitia wiki ya sheria watapata nafasi ya kuwaelimisha wananchi kuwa usuluhishi ni njia bora na rahisi katika utatuzi wa migogoro inayotumika duniani na kuwaondoa hofu kuwa kesi huchelewa kukamilika na kuchukua muda mrefu ni kwa sababu ya kufuata sheria na taratibu za usuluhishi ili uamuzi unapotolewa pande zote zipate haki.


Hata hivyo amesema kuwa katika Wilaya hiyo kwa muda mfupi waliofanya kazi wamebaini kuwa vitendo vya kujichukulia sheria mkononi, matukio ya ukatili wa kijinsia, mauaji zikiwemo mimba za utotoni ni matukio yanayo ongoza kujirudia mara kwa mara hivyo watajikita katika kutoa elimu zaidi kwa wananchi.


Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameshukuru kwa kuogezewa huduma ya sheria karibu huku wakisisitiza changamoto walizonazo hasa vitendo vya ukatili.


"Tunashukuru kwa sisi wakazi wa hapa maana changamoto tulizonazo ni nyingi sana, ukiangalia vitendo vya kikatili vinavyotendeka ni vingi sana tulikuwa tunafikiria tutayapeleka wapi malalamiko yetu"- amesema Noriath Kakuta,mkazi wa kitongoji cha Majalila.


Kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu: wajibu wa Mahakama na wadau" ambapo uzinduzi huo Kitaifa umezinduliwa Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi akiwa ni Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.


Kauli hii imebeba ujumbe muhimu kuhusu wajibu wa mahakama na wadau katika kutumia njia ya usuluhishi kutatua migogoro kwa lengo la kukuza uchumi endelevu ambapo wiki hii ya Sheria ni wakati wa Mahakama na wadau  kuwaelimisha wananchi faida za kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi.

Matangazo

  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA DEREVA II, KATIBU MAHSUSI III NA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KARATU WAFANYA ZIARA TANGANYIKA KUJINOA KUHUSU BIASHARA YA KABONI, MKURUGENZI NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI WAAHIDI MAKUBWA.

    April 08, 2025
  • WANANCHI ZAIDI YA 3700 KUONDOKANA NA CHANGAMOTO YA MAJI SAFI NA SALAMA, TANGANYIKA.

    April 09, 2025
  • MIAKA MINNE YA RAIS DKT. SAMIA, TANGANYIKA YAPOKEA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 501 UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO.

    April 14, 2025
  • WATENDAJI WA KATA & VIONGOZI WA WAFUGAJI WAPIGWA MSASA MATUMIZI BORA YA ARDHI NA UFUGAJI WA KISASA KATIKA WILAYA YA TANGANYIKA

    March 27, 2025
  • Tazama zote

video

MILIONI 328 KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA TFS TANGANYIKA, DC BUSWELU ASISITIZA UBORA WA MAJENGO.
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA TANGANYIKA
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    TONGWE - MAJALILA

    Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA

    Telephone: +255-252955264

    Simu ya mkononi: 0754870344

    Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.