Wananchi wilayani Tanganyika Mkoani Katavi wametakiwa kuendelea kumuombea, kumshukuru na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwaletea fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Onesmo Buswelu alipokuwa akihutubia wananchi wa wilaya hiyo katika maadhimisho ya Miaka Minne ya Uongozi wa Rais Samia tangu kuapiswa kwake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Katiki kipindi hiki cha miaka minne ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wilaya yetu imekuwa miongoni mwa wilaya ambazo zimenufaika kwa kupata fedha nyingi sana za miradi ya maendeleo, hivyo ni muhimu tuendelee kumuombea, kumshukuru na kumuunga mkono Rais wetu ili azidi kuleta fedha nyingi na miradi mingine ya maendeleo” amesema DC
Buswelu.
Mheshimiwa Buswelu ameongeza kwa kusema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi thabiti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kutekelezwa wilayani Tanganyika ili maisha ya wananchi wilayani humo yazidi kuinuka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Hamad Mapengo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi ambazo zimesaidia halmashauri hiyo kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule za msingi mpya 30 katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.
Aidha, Mheshimiwa Mapengo amemuoma Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kushusha fedha ili kukamilisha miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ikiwemo ya Maji, Umeme, Barabara, Elimu na Afya.
Wilaya ya Tanganyika imenufaika kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Rais Dkt. Samia kwa kipindi cha miaka minne kwani katika kipindi hicho, wilaya hiyo imepokea fedha zaidi ya shilingi bilioni 501 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.