Katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Zahanati ya Lugonesi iliyopo Kata ya Mwese, Mkuu wa Mkoa aliwakilishwa na Mhe. Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, tukio hili limefanyika tarehe 19/09/2022 likihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Tanganyika Ndugu Shaban Juma, Mkurugenzi wa Kaboni Tanzania Ndugui......pamoja na Mkurugenzi wa Tuungane Mr. Lukindo Hiza.
Katika taarifa yake, alilishukuru shirika la Tuungane kwa kazi wanazozifanya za utunzaji wa Mazingira. ‘Mumetoa Elimu ya Matumizi bora ya ardhi, pamoja na upandaji wa miti ya mbao na mikorosho mukilenga kupunguza utegemezi kwenye rasilimali ya miti ya asili na kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja’. Alisema Mhe. Buswelu.
Ujenzi wa zahanati ya Lugonesi umefadhiliwa na Mradi uitwao Tuungane kwa Afya na mazingira bora, pia Afisa Maliasili wa Wilaya ya Tanganyika Ndg Bruno Mwaisaka alitoa ufafanuzi wa namna Wilaya ya Tanganyika ilivyonufaika na Mradi huo.
Mradi wa Tuungane kwa Afya na Mazingira bora umefanikiwa kuwezessha mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji 12 vyenye baionui muhimu ya kuhifadhiwa kama vile Sokwe mtu, kiumbe ambacho kipo hatarini kupotea Duniani.
Pia mradi umewezesha kufadhili vijana 56 kupata mafunzo ya ulinzi wa misitu na Wanyamapori katika chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Kilichopo katika Jijii la Mwanza. Aidha mradi umewezesha kutoa vifaa mbalimbali vya ufugaji wa nyuki katika vijiji nane vya biashara ya hewa ukaa, vifaa hivyo ni mizinga 200, machujio 50 pamoja na nguo maalumu 50 za kuvaa wakati wa kuvuna asali.
Na mradi umesadia upandaji wa miti ya mbao na mikorosho kwa ujumla ni milioni nne, ukilenga kupunguza utegemezi kwenye rasilimali ya miti ya asili na kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja. pia kuwezesha ngazi za vijiji kupata mafunzo ya utawala bora katika usimamizi wa rasilimali maliasili za vijiji,aidha kupitia mafunzo hayo ilipelekea kuanzishwa kwa taasisi ya JUMIMIMNTA amabyo imekuwa ni mhimili mkubwa katika usimamizi wa misitu iliyopo kwenye biashara ya Hewa ukaa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.