Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mh. Suleiman Moshi Kakoso amewataka wazazi wilayani Tanganyika kuhakikisha wanasimamia vyema suala la maadili kwa watoto ili kuweza kuwanusuru na janga la mmomonyoko wa maadili,
Mheshimiwa Kakoso ameyasema hayo jana alipoalikwa kuhudhuria Baraza la Eid lililoandaliwa na Bakwata wilaya ya Tanganyika lililofanyika katika viwanja vya sule ya msingi Mpandandogo,
“Nawaomba sana wazazi wenzangu tulivalie njuga suala la maadili kwa watoto wetu, sikuhizi kuna wimbi la kubwa la mmomonyoko wa maadili hivyo tusimame imara katika hilo” alisema Mh. Kakoso,
Mheshimiwa Kakoso pia aliongeza kwa kuwataka waislamu kufanyakazi kwa bidii na kujitoa ili kuweza kuijenga dini na kujenga taasisi mbalimbali zitakazonufaisha baraza na waislamu kwa ujumla wake kama vile shule, vituo vya afya na miradi mingine,
Aidha mheshimiwa huyo aliwahakikishia waumini wa kiislamu na viongozi wa Bakwata wilayani Tanganyika kuwa yupo pamoja nao na atawaunga mkono kwa kadri watakavyoona inafaa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.