Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika ambae pia ni Diwani wa Kata ya Mpanda Ndogo Mh. Hamad Mapengo ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo,
Mheshimiwa Mapengo ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya wilaya ya Chama cha Mapinduzi ya ukaguzi wa miradi na usikilizaji wa kero za wananchi.
“Tunaipongeza na kuishukuru serikali yetu kwa kuendelea kutupatia fedha nyingi ambazo zimetuwezesha kutekeleza miradi mingi hapa wilayani kwetu” alisema Mh. Mapengo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.