Madiwani wa Halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi wamekubali mpango wa Serikali wa kupumzisha uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa muda wa kipindi cha miezi mitatu.
Hayo yamejiri katika kikao maalumu kilichowakutanisha timu ya Wizara ya mifugo na uvuvi, viongozi wa halmashauri ya Tanganyika, watendaji kata, vijiji na maafisa uvuvi katika ukumbi wa Halmashauri ya Tanganyika.
Wakizungumzia juu ya utekelezaji wa upumzishaji shughuli za uvuvi ziwa Tanganyika, diwani wa kata ya Karema Michael Kapata na diwani wa kata ya Ikola wamesema wazo hilo ni zuri kwani ni ukweli usiopingika kuwa samaki katika ziwa Tanganyika wamepungua tofauti na kipindi cha nyuma.
Naye mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wataalamu wa kilimo kuandaa maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo ili wakazi waeneo hilo wawe na namna nzuri ya kujiingizia kipato tofauti na uvuvi wakati zoezi la usitishwaji likiendelea.
Kwa upande wake Masui Munda, mteknolojia wa samaki mwandamizi ambaye ni afisa dawati wa ziwa Tanganyika amesema zoezi hilo litaenda sambamba na kubaini nyavu haramu ili zisiendelee kutumika.
Zoezi la upumzishaji shughuli za uvuvi ziwa Tanganyika linatarajia kutekelezwa tarehe 15 mwezi wa Nne mwaka huu hadi tarehe 15 mwezi wa Nane mwaka huu.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.