Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi leo imewapokea madaktari bingwa kutoka nchini Marekani wanaokuja wilayani humo kwa ajili ya kutoa huduma za upasuaji wa magonjwa mbalimbali BURE kabisa bila malipo yoyote,
Mapokezi hayo makubwa yaliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mh. Shaban Juma ambae aliongozana na wakuu wa idara mbalimbali wa Halmashauri hiyo,
Miongoni mwa magonjwa ambayo yatapatiwa matibabu ni pamoja na Goita, Ngiri/Hernia, Uvimbe kwenye ngozi, Uvimbe kwenye kichwa, Uvimbe kwenye mfumo wa uzazi, Makovu sugu na mengine,
Halmashauri inawaalika wananchi wote wa wilaya ya Tanganyika na maeneo jirani kuweza kuhudhuria na kupata huduma mbalimbali zinazokwenda kutolewa kuanzia tarehe 6-13.04.2024.
WOTE MNAKARIBISHWA.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.