Wadau wa Habari wa mkoani Katavi wamejengewa uwezo wa kukuhamasisha wasichana wa miaka 14 kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa shingo la kizazi. Chanjo hiyo inajulikana kwa jina la ‘HPV vaccine’ ambayo ina uwezo wa kumlinda binti asipate saratani ya mlango wa shingo la kizazi.
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Omary Sukari Aprili 17, 2018 katika ukumbi wa Mkuu wa wilaya ya Mpanda.
Aidha Dkt. Sukari amesema kuwa chanjo hiyo inatolewa bila malipo yeyote. Wasichana wate waliotimiza miaka 14 watapatiwa dozi na watarudia baada ya miezi sita.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.