Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Albert Msovela amempongeza Afisa Elimu Mkoa na timu yake kwa usimamizi mzuri wa ufundishaji na usimamizi wa elimu uliopelekea ufaulu kwa asilimia mia moja kwa wanafunzi wa kidato cha sita licha ya changmoto zilizopo.
Msovela ameyasema hayo leo katika kikao kazi cha Maafisa Elimu Kata wa Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika ukumbi wa Kichangani Manispaa ya Mpanda kilichowakutanisha Maafisa Elimu Kata wa Mkoa wa Katavi ili kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendesha sekta ya Elimu Mkoani hapa.
Aidha Msovela ametoa wito kwa Maafisa Elimu Kata wote kuhakikisha wanasimamia na kufanya majukumu yao kwa weledi na kusimamia kwa ukaribu ili kuwezesha ufaulu zaidi Mkoani hapa.
Kwa Upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Katavi, Upendo Rweyemamu amesea kuwa kikao hicho kimelenga kukumbushana kuhusu majukumu ya kazi na kuelimishana juu ya usimamizi mzuri wa elimu ili kufanya vizuri zaidi.
Bi. Rweyemamu ametoa wito kwa Maafisa Elimu Kata kuhakikisha wanayafanyia kazi yale yote waliyoelekezwa katika kikao hicho ili kurahisisha wepesi wa kazi ya usimamizi wa elimu katika Kata hizo.
Kwa upande wao baadhi ya Maafisa Elimu Kata walioshiriki kikao kazi hicho, Khalid Masepo amesema kuwa kikao hicho kimeruhusu mijadala itakayo wezesha kujadiliana kwa pamoja nini cha kufanya na kuwa watakwenda kuyafanyia kazi yale yote walioelekezwa.
Kikao Kazi hicho ambacho mgeni rasmi ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kimefanyika kwa mara ya kwanza kuwakutanisha Maafisa Elimu Kata Mkoa kwa Pamoja kujadili mambo yao.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.