"NENDENI MKASHIRIKIANE WOTE KAMA WILAYA KAMA MNATAKA KUFANIKIWA KWENYE BIASHARA YA KABONI" DED SHABAN JUMA.
Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi imetakiwa kuwa na umoja na mshikamano baina ya makundi yote ndani ya jamii kama kweli inataka kufanikiwa katika biashara ya Kaboni,
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Tanganyika Bw. Shaban J. Juma wakati wa mafunzo ya biashara hiyo yaliyotolewa katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika,
Bw. Shaban Juma amesema kuwa Biashara ya Kaboni ni miongoni mwa biashara zinazoweza kuiingizia kipato kikubwa sana halmashauri yao lakini ili waweze kufanikiwa ni lazima wawe wamoja kwa kushirikisha makundi yote ndani ya jamii,
Naye, Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanganyika Bw. Lincoln Tamba aliwataka wageni hao kutoka Nachingwea kuhakikisha wanakwenda kuyatumia vyema mafunzo waliyoyapata ili waweze kufaidika na matunda ya biashara ya kaboni,
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohammed Moyo alishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa mapokezi makubwa na mazuri waliyowapa na kuahidi kwenda kutumia vyema elimu waliyoyapata ili kuwanufaisha wananchi wa Nachingwea,
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhe. Adinani Mpiyagila alishukuru kwa elimu waliyopata na kuahidi kwenda kushirikiana na Madiwani wenzake kuhakikisha Nachingwea wanaingia kwenye biashara hiyo ili waweze kusaidia kusukuma gurudumu la kuwaletea wananchi maendeleo,
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeendelea kujizolea umaarufu mkubwa kwa kutekeleza vyema biashara ya Kaboni baada ya hivi karibuni kupokea kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 14 kutokana na biashara hiyo.
@mohamed_mchengerwa @nachingwea_dc @nachingwea_fm @lindi_rs_ @carbontanzania @maelezonews @ortamisemi
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.