Wananchi wa kijiji cha Kusi kilichopo kata ya Bulamata wanahitaji lori ya kubebea mawe ya ujenzi wa zahanati ya kijiji. Hayo yamesemwa mbele ya mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mhe. Hamadi Mapengo wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa zahanati hiyo ya Juni 8, 2018.
Mwenyekiti ameahidi tatizo hilo kulitafutia ufumbuzi kwani wananchi wa kijiji cha Kusi wanajitoa sana katika shughuli za maendeleo. Naye Diwani wa viti maalum Mishamo, mhe.Sikuzani Nkolonko amesema anawaonea sana huruma wakina mama wanaobeba mawe makubwa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.