Kilimo cha pamba wilayani Tanganyika
Uchumi wa Wananchi walio wengi katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda hutegemea kilimo ambacho sehemu kubwa huendeshwa na wakulima wadogo wadogo .
Karibu asilimia 85 ya watu waishio Vijijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Mapanda hujishughulisha na kilimo, katika kutambua hilo Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbali mbali imekuwa ikitoa elimu na hamasa kuhusu ulimaji wa mazao ya chakula na biashara .
Kwa msimu wa kilimo wa 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda chini ya uongozi wa Mhe,Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando iliwahamasisha wakulima kuanza kujishughulisha na kilimo cha Pamba.
Hamasa hii ilifanyika katika Kata 14 ambazo ni Katuma,Mpandandogo,Tongwe,Sibwesa,Kasekese,Kapalamsenga Karema,Isengule,Mishamo,Bulamata,Ipwaga,Kabungu,Ilangu na Karema ambapo jumla ya wakulima 2126 walijiandikisha kulima zao hilo na takribani ekari 4798.25 zinatarajiwa kulimwa. Wakulima hawa walipata Hamasa katika mikutano mbali mbali ambayo walipata wasaa wa kuuliza maswali kwa wataalam na Viongozi juu ya faida ya kilimo cha pamba masoko upatikanaji wa Pembejeo na Viatilifu.
Katika kutambua umuhimu wa kuwa na kumbukumbu za wakulima wa zao hili ,Halmashauri iliandaa daftari la orodha ya wakulima likionesha kata na kijiji anachotoka kulima
Lengo ni kuweza kutambua mahitaji mbali mbali yatakayopelekea zao hili kulimwa kwa ufanisi,Mahitaji hayo ni uwepo wa mbegu bora, viatilifu, bomba na maafisa ugani walio na utaalam wa zao la Pamba.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.