Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanganyika Bw Lincoln Tamba, aliyeamvatana na wataalam kutoka H/W ya Tanganyika ametembelea mradi wa Barabara ya Ifinsi-Bugwe yenye urefu wa 120km, iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe na TARURA.
Katika ziara hiyo alizungumza na Wananchi wa Kitongoji cha Ifinsi na kutumia nafasi hiyo kuwakumbusha wakulima wote kulima kwa kutumia mbolea na viatilifu, ili kuongeza tija na ubora wa mazao yao.
Vilevile amewataka Wakazi wote wa eneo hilo kuzingatia kanuni na taratibu za ujezi, hivyo kuwasihi kuacha kujenga kiholela kwani kitongoji hicho kinazidi kukua kila siku.
Aidha Kaimu Meneja wa TARURA Eng. Maila Richard ambao ndio wasimamizi wa mradi huo, amewataka wananchi wote wa maeneo hayo kuacha kulima pembezoni mwa Barabara ikiwa ni pamoja na kupitisha mifugo, ili kulinda Barabara isiharibike.
Amekumbusha kuwa Mwananchi yeyote anayehitaji kulima anapaswa kuacha eneo la Barabara lenye upana wa miguu 24 ya mtu mzima kwa kila upande.
Lakini pia Baadhi ya wakazi wa Ifinsi akiwemo Mzee Shabani amemshukuru sana Mhe Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatia Barabara hiyo iliyokuwa ni kikwazo cha muda mrefu, huku wengine wakiomba kusogezewa huduma ya umeme kwani Kitongoji hicho kinazidi kukua kwa kasi.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.