JKT KUNUFAISHA WANANCHI WILAYANI TANGANYIKA .
Na Sylvanus Ntiyakenye.
Tanganyika. Halmashauri ya wilaya ya Mpanda imesaini hati ya kukabidhi eneo litakalojengwa kambi ya JKT katika wilaya ya Tanganyika. Makabidhiano hayo yamefanyika Aprili 5, 2017 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda.
Eneo lililokabidhiwa lina ukubwa wa hekta 4,000 na lipo Kaskazini mwa halmashauri ya wilaya ya Mpanda (Tanganyika). Eneo hili linapakana na msitu wa Tongwe Mashariki kwa upande wa Kaskazini, Mashariki linapakana na eneo la uwekezaji la halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Kwa upande wa Kusini linapakana na barabara ya Mpanda –Kigoma na kijiji cha Vikonge, na Magharibi eneo limepakana na makazi ya Mishamo (kata ya Bulamata).
Mipaka ya eneo hili la JKT imeanzia karibu na eneo maarufu kwa jina la ‘Pembe la ng’ombe’ katika barabara ya Mpanda-Kigoma, mkono wa kulia kama unaelekea Kigoma jira namba 256899E, 9364061N. Mpaka unafuata barabara ya Mpanda-Kigoma kuelekea Kigoma kupitia jira namba 256692E, 9364270N hadi jira namba 256100E, 9365347N.
Pia mpaka unaelekea upande wa kusini kupitia jira namba 256041E, 9365310N hadi jira namba 254209E, 9360754N. Eneo linapita katika mpaka wa makazi ya Mishamo kuelekea upande wa Magharibi-Kaskazini kupitia jira namba 254454E, 9367050N hadi makutano ya mpaka wa msitu wa hifadhi wa Tongwe Mashariki jira namba 254859E, 9377488N.
Hata hivyo, kwa upande wa Kaskazini eneo la JKT litaishia kwenye mpaka wa msitu wa hifadhi wa Tongwe Mashariki unapoanzia na mpaka utapita katika jira namba 254944E, 9377262N, 255184E, 9376998N, 255544E, 9376782N,255712E, 9376734N, 255880E, 9376806N, 255976E, 9376398N, 255808E, 9375822N, 255832E, 9375462N, 256022E, 9375105N, 256239E, 9374165N, 256575E, 9373733N, 256671E, 9373158N, 256750E, 9372251N, 256894E.
Jira zingini ni namba 9371722N, 257302E, 9371098N, 257686E, 9370018N, 258358E, 9368747N,258598E, 9367954N, 258838E, 9367690N, 259222E, 9367402N, 259294E, 9367235N, 259390E, 9366827N hadi jira namba 259461E, 9366756N. Mpaka utaekea Kusini hadi jira namba 256899E, 9364061N mpaka ulipoanzia.
Faida watakazopata wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda(Tanganyika) kutokana na JKT;
Mkuu wa jeshi la JKT Meja Jenerali Michael Isamuhyo amesema, “zipo faida nyingi ambazo wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda watanufaika nazo”. Mojawapo ni kuimarisha ulinzi na usalama kwa mipaka ya halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Ulinzi ukiimalika, halmashauri itakusanya mapato yaliyokuwa yanatoroshwa na kwa njia za panya.
Pia Isamuhyo aliongeza kwa kusema, “JKT ina watalaam wa fani mbali mbali. Mfano walimua au madaktari watakuwa wanatoa huduma kwa vijiji vilivyo jirani na kambi hii kwa gharama za JKT”. Walimu wa JKT wataenda kufundisha wanafunzi wa halmashauri ya Mpanda kwa gharama za JKT. JKT itajenga kituo cha Afya katika kambi ila wananchi wa vijiji vinavyozunguka kambi hiyo watakuwa wanapata matibabu bure.
JKT watakuwa na mashamba darasa ya kilimo na mifugo, hivyo wananchi watapata fursa ya kujifunza kuendesha kilimo na ufugaji bila kuathili mazingira. JKT wataendesha kilimo cha umwagiliaji na kuwa walimu wazuri kwa wakazi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda.
Kwa kuwa tayari kuna kambi ya JKT, vijana wengi wa kutoka Tanganyika watapewa nafasi nyingi za kujiunga na jeshi hilo.
Naye Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amewapongeza JKT kwa kuanzisha kambi katika wilaya ya Tanganyika. Kuwepo kwa kambi ya Jeshi, kutasaidia kuinua uchumi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwani zile mbao zilizokuwa zinatoroshwa kuelekea Uvinza, Kigoma ama Tabora zitaanza kulipiwa ushuru.” Mazao ya misitu yataanza kuwanufaisha wananchi wa wilaya ya Tanganyika”, alisema Muhuga.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mhe.Hamadi Mapengo ameshauri JKT kuwa na mahusiano mazuri na wananchi. Lengo la kuanzisha kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa katika wilaya ya Tanganyika liwe kweli kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya ya Tanganyika, na siyo uwanja wa kupiga na kuwanynayasa wananchi wanaozunguka maeneo hayo. “Isifikie mahala ambapo sisi wawakilishi wa wananchi tunashindwa kuwafikia kambini kutokana na adhabu za kijeshi”, alisema Mhe. Mapengo
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) liliomba ardhi kwa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo na mifugo na ardhi ya kujenga kambi ya JKT. Vikao vya baraza la madiwani wa halmashauri vilipitisha azimio kuwa ardhi hiyo ikabidhiwe kwa JKT. Tayari ardhi hiyo imekabidhiwa kwa JKT mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga, Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Bw. Salehe Mhando, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mhe. Hamadi Mapengo pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw.Romuli John na ujumbe wake.
Kwa upande wa JKT alikuwepo Mkurugenzi Mtendaji SUMA-JKT Brigedia Jenerali Charo Yateri na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Michael Isamuhyo na ujumbe wake.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.