Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Tanganyika imekutana kufanya majumuisho ya ziara iliyofanyika siku tatu kuanzia Desemba 11-12 katika maeneo mbalimbali yenye miradi Wilayani humu.
Kikao hicho kiliwakutanisha Viongozi wakubwa wa kisiasa na wataalam wa idara na vitengo vya H/W ya Tanganyika, ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Yasin Kibiriti aliongoza, kikao hicho akiwemo Kamisaa wa Kamati ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe Onesmo Buswelu.
Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa ni Ufuatiliaji wa ujenzi wa matundu mawili ya vyoo shule ya Msingi Ikola, Ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Karema, huku baadhi ya miradi kama barabara na nyumba za Watumishi zikipewa kipaumbele katika utekelezaji.
Mkuu wa Wilaya Mhe Buswelu amesema kwamba yeyote atakayejitokeza kukwamisha miradi ya maendeleo atachukuliwa hatua.
“ Uchunguzi wa Mkaguzi wa ndani unaendelea utakapokamilika tutakaa vikao vyetu, na hatua za kisheria zitachukuliwa. Pia haimaanishi akiondoka mtumishi mmoja Mtendaji wa Kata au Kijiji, kazi ya utekelezaji wa miradi lazima uendelee” DC Buswelu.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.