Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanganyika ikiongozwa na Mwenyekiti wake Yasin Kiberiti Jana Januari 23,2023 imeanza ziara ya siku tano ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.
Wakiwa katika mradi wa ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika kituo cha Afya Ipwaga, Mwenyekiti Kiberiti amesema ameridhishwa na hatua ambayo miradi yote waliyotembelea imefikia huku akisisitiza usimamizi zaidi ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.
Aidha, ametoa wito kwa viongozi ambao ni wasaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kusimamia Ilani ya CCM kwa kile alichodai dhamira ya chama hicho ni kuhakikisha wananchi wanafaidi matunda ya chama hicho.
"Serikali yetu iko makini na ni jukumu letu Chama Cha Mapinduzi kuisimamia Serikali na kuishauri"
Pia ameshauri halmashauri kusaidia fedha ili kuboresha ujenzi wa mradi wa Zahanati Kijiji cha Kapemba unaotekelezwa kwa fedha za mfuko wa jimbo ambao toka mwaka 2017 mradi uanze kujengwa hadi sasa mradi huo umekwama katika hatua za umaliziaji.
Kwa upande wake mwakilishi wa mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambaye pia ni Afisa mipango Deus Luziga amesema Halmashauri iko tayari kuwaunga mkono wananchi katika miradi iliyoanzishwa kwa nguvu zao endapo watazingatia utaratibu wa kufikisha mradi hatua ya lenta.
Kamati hiyo jana imetembelea mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mganga Kijiji cha Kapemba wenye thamani ya Tsh. Milioni 50 sambamba na ujenzi wa mradi wa zahanati ya Kijiji hicho, ujenzi wa mradi wa maji vijiji vya Isenga, Ifumbura na Kapemba unaoghalimu zaidi ya Tsh. Bilioni 1.3, mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Isubangala.
Miradi mingine ni ujenzi wa Zahanati ya Kijiji Mganza iliyoibuliwa kwa michango ya Wananchi na mradi wa ujenzi wa jemgo la wagonjwa wa nje (OPD) katika kituo cha afya Ipwaga.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.