Kamati ya Mwenge Mkoa wa Katavi ikiambatana na KUU Wilaya chini ya Mhe Mkuu wa Wilaya Onesmo Buswelu, timu ya wataalam ya Halmashauri imefanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Tanganyika lengo ni kukagua maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, unaotarajiwa kupokelewa mnamo September 23, 2025.
Katika ziara hiyo imeweza kutembelea maeneo ambayo mbio za Mwenge wa Uhuru zitapita, ikiwa ni kutembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi iliyokamilika.
Ziara hii imejikita katika kuboresha mapungufu yaliyobainika ambapo imefanyika pia hamasa kwa wananchi wa maeneo yote, ili waweze kujiandaa na kuupokea Mwenge wa Uhuru utakapofika. Maeneo yaliyofikiwa na ziara hiyo, ni Kikundi cha Vijana cha Bodaboda na Samia kilichopo Kibo-Ifukutwa, mradi wa ujenzi wa Barabara za Majalila kwa kiwango cha lami ambao umefikia asilimia 28, bweni la wasichana shule ya Sekondari Majalila lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 120, Zahanati ya Kijiji cha Vikonge, eneo la lishe bora, tume ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU).
Lakini pia ziara hiyo ilifika ukanda wa mishamo kukagua eneo linalotegemewa kuupokea Mwenge, na kukagua mradi wa maji safi na salama uliopo Kijiji cha Mazwe.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe Onesmo Buswelu ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wilayani Tanganyika, kujitokeza kwa wingi kuuraki Mwenge, ikiwa ni pamoja na kuwasihi kuvuta maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme kwa wakazi wa Kata ya Mazwe.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.