Mbunge wa Jimbo la Mpanda vijijini Mhe. Moshi Kakoso ameishsuri Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kuweka umakini katika ushuru wa mazao kwa kile alichodai Halmashauri inapoteza mapato eneo hilo.
Kakoso ametoa ushauri huo jana katika kikao cha ushauri cha Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika (DCC) ambapo kikao hicho pamoja na mambo mengine kilipitisha bajeti ya mwaka 2024/2025 ya Halmashauri hiyo ya shilingi bilioni 33.7
Aidha, ameshauri kuona namna nzuri ya kukusanya mapato eneo la Kampemba ambako kunazalishwa kwa wingi maharage na mahindi lakini licha ya eneo hilo kuingiliana na Halmashauri ya Tanganyika lakini wanaufaika wa mapato ni Halmashauri ya Nsimbo halikadharika eneo la Senta Maria ambako kunazalishwa mpunga lakini wanufaika ni Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
"Tusifikirie tu kwamba mpaka tuweke mageti, tutafute njia nyingine ya kudhibiti yale mapato kwenye wilaya vinginevyo tutakuwa tunawanufaisha wenzetu wakati ardhi ni ya kwetu"
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikao hicho, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Alhaj Majid Mwanga ameshauri kuwa na jicho la tatu eneo la afya kwani pamoja na makadirio ya mapato yanayopatikana bado nguvu ikiongezwa Halmashauri inaweza kupata fedha zaidi ya kile kinachokusanywa sasa.
"Mnapaswa kwenda zaidi ya milioni mia tano wala sio hapo mlipo kwa hiyo bado mwende mkatathimini kwa sababu kama mtatumia vizuri ule mfumo mnaweza kukusanya fedha nyingi kwa upande wa afya kwa sababu mna maduka, mna vituo vya afya, mna Zahanati na zote zina mfumo"
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.