Jumuiya ya Uhifadhi wa Misitu ya Milima ya Ntakanta (JUMIMINTA) iliyopo kwenye Vijiji 8 vinavyonufaika na Biashara ya Carbon Wilayani Tanganyika imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu biashara hiyo kwani imekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi Wilayani Tanganyika,
Shukrani hizo zimetolewa na Katibu wa Jumuiya hiyo Bw. Said Wambali alipokuwa akizungumza mara baada ya kushiriki Kilele cha Wiki ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo kitaifa kilifanyika Mkoani Katavi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuwa Mgeni Rasmi,
Bwana Wambali aliongeza kwa kusema kuwa Jumuiya yao itaendelea kuhamasisha uhifadhi na utunzaji wa Misitu ili wananchi kupitia Biashara ya Carbon waendelee kufaidi matunda ya biashara hiyo,
Kwa upande wake Mjumbe wa Jumiminta Bi. Mariam Ismail ambae pia ni Mtendaji wa Kijiji cha Mwese amemshukuru Mheshimiwa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini na Waheshimiwa Madiwani kwa ushirikiano wao uliopelekea kutekelezwa vyema kwa biashara ya Carbon,
Mwisho, Wanajumuiya ya Jumiminta kwa umoja wao wamewataka wananchi Wilayani Tanganyika na Tanzania kwa ujumla kutunza misitu iliyopo ili nayo iweze kuwatunza kwa kuwapatia kipato na kukuza uchumi.
@carbontanzania @samia_suluhu_hassan @maelezonews @mohamed_mchengerwa @ortamisemi @mkoa_katavi
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.