Tume Huru ya Uchaguzi hii leo Mei 12, imetangaza rasmi kuongeza majimbo ya uchaguzi na kubadilisha majina ya majimbo baadhi ya uchaguzi ikiwemo Jimbo la Mpanda vijijini linalopatikana Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Akitangaza mabadiliko hayo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amelibadilisha jina la Jimbo la uchaguzi la Mpanda Vijijini na sasa litafahamika kama Jimbo la uchaguzi la Tanganyika.
“Mkoa wa Katavi Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, jimbo la uchaguzi la Mpanda Vijijini limebadilishwa jina na sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Tanganyika” Jaji Mwambegele.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.