Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika imeadhimishwa Kimkoa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, ambapo Mkuu wa Wilaya wa Mpanda Jamila Kimaro kwa niaba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe Mwanamvua Mrindoko, ameitaka jamii kuwalinda watoto kwakuwa hao ndiyo nguzo muhimu ya kesho, na kutoa taarifa zozote za vitendo vya ukatili kwa watoto.
Akizungumza na wananchi katika uwanja wa Shule ya Msingi Mpanda ndogo ambapo maadhimisho hayo yamefanyika, Mhe Jamila amesema kwamba jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto, wanapatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu, afya, mahitaji muhimu, upendo, na kulindwa ili kuwawezesha kutumiza ndoto zao.
Pia ametumia nafasi hiyo kuihasa jamii kutojihusisha na unyanyasi kwa watoto, sambamba na hilo amezungumzia suala la kuendelea kulinda Amani na upendo wakati huu nchi yetu ya Tanzania, inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais.
Kwa upande wa mwenyeji wa maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya wa Tanganyika, Mhe Onesmo Buswelu ameweka msisitizo juu ya jamii kutambua nafasi ya watoto huku akitanabaisha kuwa Serikali ndiyo mlezi wao inayoshirikiana na wazazi wao, tunawakumbusha watoto wasishawishe na kudanganywa ili kuharibu Amani hii, bali waiombee nchi hii iwe na Amani na upendo.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Maria Lupunza mwanafunzi wa shule ya sekondari Kakoso, amezitaja changamoto ambazo watoto wanapitia ikiwemo kunyimwa haki ya msingi ya kusoma, malezi ya wazazi, ubakaji, na chagulaga ambayo ni mila inayopelekea binti mdogo kuingia kwenye ndoa.
Kila mwaka ifikapo Juni 16, Afrika huadhimisha siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika ikiwa ni kumbukizi ya mauaji ya watoto katika mji wa Soweto nchini Afrika Kusini, ambao waliuliwa na Serikali ya makaburu wakati wakidai haki zao.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.