✍️ Muonekano wa picha za juu (Drone Shots) wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika ambayo imekamilika na inatoa huduma za kitabibu ikiwa na vifaa vingi vya kisasa. Mradi huu umetumia kiasi cha Tsh Bilioni 3.48.
✍️ Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea, kutanua wigo wa huduma za afya kila maeneo, ambapo huduma za afya kwa sasa zimezidi kuimarika mpaka kwenye vituo vya afya vilivyopo vijijini.
✍️ Katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika huduma za afya zimeimarika, hadi sasa kuna vituo 43 vya kutolea huduma za afya:
✍️ Hospitali moja ya Wilaya, Zahanati za Vijiji 36 na vituo vya afya 6.
✍️Kwa mwaka huu Halmashauri inategemea kufungua vituo vya afya 3, na Zahanati 3.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.