HII NDIO MIRADI NANE ILIO ING'ARISHA WILAYA YA TANGANYIKA MBIO ZA MWENGE TAIFA 2025
Tanganyika, Katavi | Septemba 23, 2025 – Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko Hoza, ameongoza hafla ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Kimkoa, ambapo Mwenge huo umepokelewa rasmi katika Wilaya ya Tanganyika na kukimbizwa umbali wa kilomita 166, ukitembelea na kuzindua jumla ya miradi 8 yenye thamani ya shilingi Bilioni 2,585,436,469/=.
MIRADI ILIOZINDULIWA WILAYA YA TANGANYIKA.
Uzinduzi wa Mradi wa Maji Mazwe
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ali Ussi, amezindua Mradi wa Maji Mazwe uliogharimu Tsh Milioni 307.67. Mradi huu ni mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Kijiji cha Mazwe, waliokuwa wakitembea zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma ya maji safi na salama. Wananchi wameeleza kufurahishwa na mradi huo ambao unatarajiwa kumaliza kabisa adha hiyo ya muda mrefu.
Mapambano Dhidi ya Rushwa – Klabu ya Wanafunzi
Mwenge pia umezindua Klabu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika Shule ya Msingi Luhafwe. Mradi huu umetajwa kuwa chachu katika kuimarisha uelewa wa watoto kuhusu madhara ya rushwa. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Kiongozi wa Mbio za Mwenge alisema:
“Watoto wanapoanza kuelewa tangu wakiwa wadogo kuwa jambo fulani si sahihi, hujengewa msingi imara wa maadili. Nawasihi walimu na wazazi kuendelea kuwapa elimu ili wawe mabalozi wazuri wa mapambano dhidi ya rushwa.”
Lishe Bora kwa wanafunzi
Katika shule hiyo hiyo, Mwenge wa Uhuru umezindua Klabu ya Lishe inayolenga kuimarisha afya na lishe kwa wanafunzi. Takwimu za mkoa zinaonyesha mafanikio katika sekta hiyo ambapo hali bora ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano imeongezeka hadi 32.2% kutoka 38.4% mwaka 2015/2016.
Miradi Mingine 5 Iliyotembelewa na mwenge wa uhuru kitaifa:
Zahanati ya Kijiji cha Vikonge – inayolenga kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa kijiji hicho.
Bweni la Wasichana – Shule ya Sekondari Majalila – kuinua mazingira ya kujifunzia kwa wasichana.
Ujenzi wa Barabara za Lami – Majalila – Inayolenga uboreshwaji wa miundombinu ya usafiri.
Mradi wa Kikundi cha Vijana “Bodaboda na Samia” – kusaidia ajira kwa vijana.
Uwekaji wa Jiwe la Msingi katika ujenzi wa Barabara ya Lami yenye urefu wa kilometa nne (4).
Pia Mwenge wa uhuru kitaifa katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya matumizi ya nishati safi na salama iliongoza zoezi la ugawaji wa mitungi ya gesi ya kupikia kwa wakazi wa Kijiji cha vikonge, hii ni katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama nchini.
Miradi hii iliyo zinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ni juhudi ya serikali ya awamu ya sita ya Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Pamoja na hayo uongozi ofisi ya mkuu wa wilaya ya Tanganyika unawashukuru wananchi na wadau wote waliojitokeza kwa namna moja au nyengine wamechangia kukamilika kwa mbio hizo za mwenge wa uhuru kitaifa katika wilaya ya Tanganyika.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.