WANANCHI 5000 KUPATIWA HATIMILIKI ZA KIMILA VIKONGE
Zaidi ya wananchi 5000 wa kijiji cha Vikonge katika Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wanatarajia kunufaika na zoezi la upimaji (ardhi ya kijiji) na utoaji wa hatimiliki za kimila za mashamba, makazi na maeneo ya taasisi.
Zoezi hili linafanywa na Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kwa kushirikiana na taasisi ya Janegoodal. Wananchi watapatiwa hatimiliki za kimila bure, wao wanachotakiwa kufanya ni kutoa ushirikiano wa kuonesha mipaka ya shamba lake au eneo la makazi yake linapoanzia na kuhakikisha majirani wa pande zote nne wanakuwepo wakati wa zoezi la upimaji.
Aidha, zoezi hili linawahusisha wazee zaidi ya 4 wanaojua vizuri mpango wa matumizi bora ya ardhi wa kijiji cha Vikonge kwa lengo la kuhakikisha maeneo yanayopimwa ni yale yaliyopo maeneo sahihi kwa kuzingatia mpango wa kijiji husika. Viongozi wa kijiji, kitongoji husika pamoja na mabalozi nao wanashirikishwa katika zoezi hilo.
Hii ni kuhakikisha maeneo yaliyopo nje ya mpango wa matumizi bora ya ardhi hayapimwi na kutokupewa hatimiliki za kimila za mashamba au makazi au taasisi. Maeneo kama ya milima, mito, misitu ya vijiji au maeneo tengefu ya kijiji huachwa kwa manufaa ya jamii husika.
Hatahivyo, zoezi la upimaji na utoaji wa hatimiliki za kimila za mashamba, makazi na maeneo ya taasisi limeanza Agosti 2, 2021 na linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Septemba, 2021. Kijiji cha vikonge kina vitongoji 4 ambayo ni Mnyamasi A, Mnyamasi Kasenga, Vikonge na Mnyamasi B. Hadi sasa zoezi limeshafanyika katika vitongoji vya Mnyamasi A (Ifinsi), Mnyamasi Kasenga (Magorofani) na sasa watalaam wanaendelea na zoezi katika kitongoji cha Vikonge. Zoezi litahitimishwa katika kitongoji cha Mnyamasi B mara tu baada ya kuwahudumia wananchi wa kitongoji cha Vikonge.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.