Halmashauri ya wilaya ya Mpanda (Tanganyika ) kwa kushirikiana na wadau wa taasisi ya Jane Goodall wamekamilsha hati za hakimiliki za kimila 60 za mashamba. Mashamba hayo ya wananchi wa kijiji cha Vikonge yamepimwa na kufanyiwa mchakato wa kukamilika kwa hati hizo kwa gharama za halmashauri ya wilaya ya Mpanda pamoja na wafadhili (JGI).
Zoezi hilo lilianza mwanzoni mwa Septemba, 2018 na kukamilika Septemba 26, 2018 na leo Septemba 27,2018 wananchi wa vikonge wanakabidhiwa hati za hakimiliki za kimila katika ofisi ya kijiji.
Wananchi hawakuchangia gharama za upimaji wa maeneo yao isipokuwa watachangia shilingi 5,000 kwa mwaka kwa kila hati kama ada ya ardhi. Fedha hizo zitalipwa katika ofisi ya kijiji kwa ajili ya maendeleo ya kijiji.
“Tumeanza kumilikisha mashamba ya wananchi wa Vikonge kwa kuwaandalia hati za hakimiliki za kimila ili kuwalindi dhidi ya wavamizi wa mashamba. Tumeanza na vijiji vyote vilivyofanyiwa matumizi bora ya ardhi. Vikonge tumefanya kwa awamu ya kwanza kwa kuanza na mashamba 60 na baadaye tutaendelea na awamu ya pili ambapo tutatoa hati zaidi ya 500 na hatimaye kukamilisha mpango mzima”. Alisema ofisa ardhi mteule Bw. Musa Segeja
Hata hivyo, Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina vijiji 55 na kati ya hivyo, vijiji 23 vimefanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi na tayari vijiji vya Mnyagala, Nkungwi na Vikonge mianza kunufaika na umilikishwaji wa hati za hakimiliki za kimila. Kwa sasa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda inaendelea kuwahamasisha wananchi kuchangia gharama za hati za hakimiliki za kimila. Kwa vijiji ambavyo havina ufadhili, kila mwananchi anayehitaji hati ya hakimiliki ya kimila atachangia shilingi 50,000 kwa kila hati.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.