Wananchi wa vijiji vya Mnyagala na Nkungwi wanatarajia kumaliza tatizo la wavamizi wa mashamba pori na maeneo ya makazi baada ya kukubaliana kuanza kuwa na hati za kimila.
Mpango wa kuanza utoaji wa hati za kimila umeanza Juni 12, 2018 kwa kufanya mikutano ya hadhara ya kuwajengea uwezo wa kuelewa faida za hati.
Afisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Musa Segeja alisema, unapokuwa na eneo lililopimwa na kupewa hati ndipo unaweza kusema inaishi katika eneo sahihi. Pia unaweza kutumia hati ya kiwanja au shamba kuombea mkopo wa kibiashara au wa shughuli zingine.
Wananchi walipongeza mpango huo wa utoaji wa hati za kimila ili kuondoa migogoro ya ardhi inayosababishwa na wavamizi wa maeneo kwa kudai wao ndio waanzilishi wa eneo flani.
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina vijiji 55 na kati ya hivyo, vijiji 23 vimefanyiwa matumizi bora ya ardhi ijapokuwa bado kuna mwingiliano wa matumizi ya ardhi tofauti na mpango wake. Eneo la kilimo unakuta kuna watu wanaweka makazi na eneo la ufugaji unakuta kuna wengine wanavamia na kuendesha shughuli zingine.
Ujio wa hati za kimila ndio mwarobaini wa migogoro ya ardhi na wavamizi wa maeneo tengefu. Hati hizo zitatolewa kwa gharama ya shilingi 50,000 kwa kila eneo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.