Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imefanya kikao cha Lishe chenye lengo la kuweka mikakati madhubuti ili kuboresha suala la lishe kwenye jamii, sambamba na kikao hicho kulikuwa na ajenda mbili ikiwemo cha Tathimini ya Mwenge wa Uhuru 2024/2025.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe Onesmo Buswelu amesimamia kikao hicho kilichoazimia mambo kadhaa ikiwemo; Kuanzisha kikosi kazi cha Lishe, Kushirikiana na makampuni ya simu kutuma jumbe za kuimarisha lishe, Kuanzisha klabu za lishe mashuleni, Kuanzisha bustani za mboga na matunda shuleni na kila kaya na Kila shule kuwa na mradi wa ufugaji wa
kuku na ng’ombe wa maziwa,
Aidha Mhe Buswelu alitoa onyo kali la kuepukana na vitendo vya upigaji kwa watumishi wenye miradi,
“Watendaji wa Kata na wote wenye msishiriki katika kuhujumu miradi iliyopo kwenye maeneo yenu, naomba kila mmoja kwenye miradi yake aheshimu hizo fedha ni za Wananchi” DC Buswelu
Mhe Hamad Mapengo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika aliwakumbusha watendaji kuzingatia sheria ndogo za vijiji ili kuimarisha utunzaji wa mifugo ambayo imekuwa kero kubwa kwa wananchi,
“Niombe tu kila mtu kwenye nafasi yake akafamye kazi iliyotukuka, na hili suala la lishe ni ajenda endelevu na nishauri kwenye ufugaji wa ng’ombe na bustani za mbogamboga lakini kwenye utunzaji wa mifugo watendaji wa kata na vijiji waende kusimamia sheria ndogo za vijiji ili kuimarisha utunzaji wa mifugo” Mhe Hamad Mapengo- M/kiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,
Kwa upande wa Afisa Utumishi ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa H/W ya Tanganyika alisema,
“Lishe ni ajenda ya kitaifa inapaswa tuungane kwa pamoja na kutimiza majukum yetu, kusimamia na kuhakikisha jamii yetu iwe na lishe bora” Jane Isarara- Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.