Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeendelea kufanya vizuri katika hesabu na matumizi sahihi ya fedha ambapo kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 inefanikiwa kupata hati safi baada ya ukaguzi wa hesabu za serikali kutoka ofisi ya CAG.
Akitaja mafanikio hayo, mkaguzi wa hesabu za Serikali kutoka ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG, Ndugu CPA Kasea Lyoba ameipongeza Halmashauri, mbele ya Baraza maalum la kujadili hoja za CAG.
Akimuwakilisha Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Mwanamvua Mrindoko, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Albert Msovela amewataka watumishi wa Halmashauri kuwa na uzalendo, kuwajibika, kujitoa ili kutimiza wajibu na majukumu yao ya kazi, ili kuondoa hoja zisizo na msingi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Diwani Hamad Mapengo, ameishukuru Halmashauri, Baraza la madiwani, ofisi wa mkuu wa wilaya, watumishi wa Halmashauri na ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuwa mstari wa mbele katika kutumiza wajibu wa kiutendaji katika nafasi mbalimbali.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe Onesmo Buswelu, amesema kuwa amemshukuru, Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi mbalimbali, iliyotekelezwa, na inayoendelea kutekelezwa kwa kipindi chote cha miaka minne akiwa madarakani.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.