Madakitari bingwa 18 kutoka Marekani wanatarajiwa kuwasili Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kwa ajili ya kutoa matibabu ya kibingwa.
Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tanganyika, Shabani Juma amesema halmashauri hiyo kwa kushirikiana na shirika la The Norbert and Friends Mission (NFM-BRIGHT) wanaleta madaktari hao bingwa wataokuja kwa makundi mawili ambapo kundi la kwanza litawassili Aprili 6 mwaka huu na kundi la pili litawasili Mei 4 mwaka huu.
Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la The Norbert and Friends Mission (NFM-BRIGHT), Joel Yalanda amesema lengo la shirika hilo ni kuisaidia Serikali kutotumia pesa nyingi katika kutoa matibabu.
“Kwa kutambua mzigo unaobebwa na Serikali yetu tumeona tushiriki pamoja katika kupunguzia mzigo Serikali kwa kutumia fedha nyingi kwenye upande wa upasuaji ambao imekuwa ni changamoto kwa jamii yetu”
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Dr. Alex Mrema amesema maandalizi ya kuwapokea wagonjwa yapo vizuri na katika kipindi chote cha uwepo wa Madaktari hao huduma zitakuwa zinaanza kutolewa kuanzia saa moja asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
“Huduma hizi za upasuaji kwa Halmashauri ya Tanganyika ni za muhimu kutokana na kwamba jeografia ya Halmashauri yetu ni kubwa lakini hakuna wataalamu wa upasuaji ndani ya Halmashauri yetu na wilaya yetu”
Madaktari hao, watatoa huduma kwa watoto na watu wazima bila malipo, na baadhi ya huduma hizo ni upasuaji wa uvimbe na saratani ya matiti, upasuaji wa eneo la tumbo, upasuaji wa uso na kichwa, upasuaji wa masikio, pua na koo na upasuaji wa Ini.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.