Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Bw. Juma Hokororo ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa kuwapatia elimu bora inayokwenda kuwasaidia kutekeleza vyema biashara ya Kaboni,
Bw. Hokororo ameyasema hayo leo mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya biashara ya Kaboni yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika na kuongozwa na Mkuu wa Idara ya Maliasili na Mazingira Bw. Bruno Nicholaus,
Bw. Hokororo ameongeza kwa kusema kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inayo nia thabiti ya kuongeza vyanzo vya mapato ili kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo biashara ya Kaboni itakwenda kuwaongezea vyanzo vingine vya mapato kwa halmashauri hiyo,
“Tunashukuru sana watu wa Tanganyika kwa mapokezi mazuri lakini pia kwa elimu hii muhimu ambayo mmetupatia ambayo tunaamini inakwenda kutusaidia kutanua wigo wa ukusanyaji mapato kwa halmashauri yetu endapo itafanikiwa” amesema DED Hokororo,
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mhe. John Lucian ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa kuwapa elimu nzuri na ufahamu mpana kuhusiana na biashara ya Kaboni na kuahidi kwenda kuifanyia kazi kikamilifu,
Aidha, Mkuu wa Idara ya Maliasili na Mazingira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw. Bruno Nicholaus amewakaribisha tena Karatu kuendelea kujifunza zaidi kuhusiana na Kaboni,
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeendelea kujizoea umaarufu nchini hadi nje ya nchi kwa kufanikiwa kutekeleza vyema biashara ya Kaboni na kuwezesha kuingiza mapato ya zaidi ya shilingi Bilioni 22 tangu kuanza kwa biashara hiyo mpaka sasa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.