Tangu wachaguliwe viongozi wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika hii leo wameapishwa rasmi kuzitumikia nafasi zao katika maeneo yao.Nafasi hizo ni Uenyekiti wa Kijiji na Kitongoji, Mjumbe wa Kijiji Kundi Maalum Wanawake na Mjumbe wa Kijiji Kundi Mchanganyiko.
Katika zoezi hilo la uapisho Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Shaban Juma amewapongeza na kuwataka kufanya kazi kwa bidii.
“Mimi niwapongeze sana kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi, hii ina maana kubwa sana kwenu kuwa mmeaminiwa na wananchi wenu kuwatumikia katika shughuli zote.Lakini pia niwatake kufanya kazi kwa bidii na mimi nitawapa ushirikiano wa kutosha ili kukamilisha majukumu yenu” Shaban Juma.
Aidha katika zoezi hilo liliambatana na semina fupi ya mafunzo kutoka kwa Maafisa Mbalimbali wa Serikali wakiwemo Afisa Rasilimali watu na Utawala, Afisa Wa TAKUKURU, na Afisa Uhamiaji Wilaya ya Tanganyika kwa pamoja walizungumza na viongozi hao.
“Mnapoenda kwenye ofisi zenu epukaneni na vitendo vya rushwa, fanyeni kazi kwa haki na usawa ili kila mtu apate haki yake” Kichere Mwita-Afisa TAKUKURU.
“Jambo muhimu kwa Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji ni kuwa na madaftari ya wakazi wanaoingia kwenye maeneo yenu, anapotoka na anapokwenda pamoja na majina yake halisi ni muhimu taarifa hizi zikipatikana” Mrakibu wa Uhamiaji- Elinipendo Kazael Mrisha.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.