Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw Shaban J. Juma akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika amekabidhi kiasi cha fedha taslimu shilingi 100,000/= pamoja na cheti cha kutambua na kuthamini mchango wa mtumishi bora wa mwezi Julai, 2025, ambaye ni mtumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika.
Katika tukio hilo Bw Emmanuel Kitomaga Afisa Muuguzi msaidizi amechaguliwa kuwa mtumishi bora na kupokea zawadi hiyo kama motisha ya kuongeza kasi na ufanisi wananchi kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha wakati wa kukabidhi zawadi na cheti hicho, DED Shaban amewakumbusha watumishi wote kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya utumishi na kuongeza kuwa huu ni muendelezo kwa kila Idara na Vitengo kuwatambua watumishi hodari kabla ya pasina kusubiri Mei Mosi pekee.
Kwa upande wa Afisa Utumishi Bw. Clavery Reginald amewataka watumishi wote haswa kwa upande wa afya kuzingatia maadili wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa na kutahadharisha matumizi ya simu wakati wa kazi.
Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt Alex Mrema, imeanzisha utaratibu wa kuwatambua aina mbili ya watumishi, mtumishi hodari wa mwezi na mtumishi asiye hodari ambapo, wote wawili hupatiwa zawadi kwa kuzingatia utendaji kazi wa mtumishi husika kwa mtumishi asiye hodari hupatiwa kinyago maalum kitakachokaa ofisini kwake kwa muda wa mwezi mzima mpaka pale atakapopatikana mshindi kwa upande wa mtumishi asiyekuwa hodari.
Hata hivyo vigezo vinavyotumika kubaini makundi yote mawili ya mtumishi hodari na asiye hodari ni kwa kuzingatia kujituma kazini, maadili, weledi, muda anaotumia kutoa huduma, upatikanaji wake kwa wakati, na nidhamu kazini.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.