Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe, Onesmo Buswelu amekagua maendeleo ya ujenzi wa miradi miwili inayotekelezwa kwa pesa za biashara ya Kaboni, katika Kitongoji cha Lwega namba 8B, maarufu kwa jina la Manyonyi.
Miradi hiyo ni ujenzi wa Zahanati ya kijiji wenye thamani ya Tsh Milioni 190, ambao upo hatua ya boma, na ujenzi wa nyumba moja ya walimu (2 in 1), wenye thamani ya Tsh 118, na upo hatua ya upauaji.
Katika ziara hiyo ambayo ameweka jiwe la msingi ujenzi wa nyumba ya walimu, Mhe Buswelu ameagiza ujenzi wa miradi hiyo kwenda kwa kasi ili ikamilike ndani ya wakati, huku akiagiza kamati ya ujenzi kuhakikisha fundi aliyeshinda zabuni hizo kuwepo eneo la mradi na sio kuachia vibarua na yeye kushinda mjini.
Aidha pia amemuagiza afisa tarafa wa Mwese kuhakikisha kila wiki anafika kukagua maendeleo ya miradi hiyo, sambamba na maagizo hayo pia amezitaka kamati zote za miradi kufanya kazi kwa kushirikishana ili kila mmoja awe na taarifa sahihi za mradi.
Kwa upande wa wakazi wa Kitongoji cha Lwega namba 8B, wamemshukuru sana Mhe Rais kwa kuwawezesha ujenzi wa Zahanati hiyo, kwani itapunguza kero ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.