Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Mh. Onesmo Buswelu jana aliwatembelea na kuwajulia hali wahanga wa mafuriko yaliyotokea katika eneo la Karema wilayani humo kufuatia kuongeza kwa maji katika ziwa Tanganyika hali iliyopelekea maji kuvuka kingo zake na kuelekea katika makazi ya watu,
Mheshimiwa Buswelu akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, walifika kijijini hapo na kutembelea maeneo yaliyoathirika na kuwataka wananchi kuhama maeneo hayo kwani tayari yamekuwa hatarishi kwa maisha yao,
"Tunawaomba wananchi wenzetu muweze kuhama maeneo haya kabla majanga zaidi hayajatokea kwasababu hatujui ni lini mvua zinataka, kwahiyo tuhame na kuhamia sehemu zilizo salama zaidi" alisema Mh Buswelu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika, Bw. Philemon Mwita aliwahakikishia wananchi wa Karema kuwa halmashauri kwa kushirikiana na Tarura na Ofisi ya Ardhi watafika tena Karema kwa ajili ya kuwapimia viwanja na kutengeneza miundombinu ya barabara ili kuharakisha zoezi la wananchi hao kuhamia maeneo yenye usalama zaidi,
Mafuriko hayo yameathiri kaya zaidi ya 200 na tayari serikali kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijiji Mh. Suleiman Kakoso wameanza jitihada za kuwatafutia makazi bora wananchi wa Karema.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.