Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Mh. Onesmo Buswelu ametoa muda wa siku 3 kwa Tarura wilayani humo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa kivuko katika mto Mwali ili wananchi waweze kupita bila changamoto yoyote,
Mheshimiwa Buswelu ameyasema hayo leo baada ya kutembelea na kukagua shughuli za ujenzi wa Kalvati katika mto Mwali na kubaini kuwa sehemu ya kupita wananchi wanaopisha ujenzi wa Kalvati hilo ni hatarishi kwa usalama wao na mali zao,
"Nimeona shughuli za ujenzi wa Kalvati hili zinakwenda vizuri lakini sehemu ya kupita wananchi bado ni changamoto hivyo natoa muda wa siku 3 nataka mjenge kivuko pale ili wananchi waweze kupita bila wasiwasi wowote" alisema Mh. Buswelu
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Majalila Bw. Ali Mashaka Fundi ambae ndio mwakilishi wa wananchi wa kijiji cha Majalila, amemtaka mkandarasi kuhakikisha ujenzi wa kivuko hicho unakwenda kwa haraka kwani wananchi wake wamepata tabu vya kutosha,
Kalvati la Mto Mwali lipo katika barabara inayounganisha vijiji vya Majalila na Ifinsi yenye urefu wa kilometa 18 inayojengwa kwa kiwango cha changarawe.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.