Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Onesmo Buswelu, ameendelea na ziara yake kijiji kwa kijiji akihamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Katika ziara hiyo, Mhe. Buswelu amewakumbusha wananchi wa kujiji cha Ngomalusambwa, Mchakamchaka na Igagala umuhimu wa kutumia haki yao ya kupiga kura kwa kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais wanaofaa kuleta maendeleo katika jamii zao.



Aidha, amewahimiza wakulima kutumia mbegu bora na pembejeo sahihi ili kuongeza tija katika kilimo, hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya msimu mpya. Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameidhinisha ruzuku ya mbegu zinazopatikana kwa bei nafuu ya shilingi 7,000 tu, hatua itakayowawezesha wakulima wengi kuongeza uzalishaji.
Pia, Mhe. Buswelu amekagua miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa zahanati za Mchakamchaka na Ngomalusambwa, ambapo ameahidi ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuchangia mifuko 10 ya saruji kusaidia ujenzi wa vyoo katika zahanati hizo. Amewataka pia wakandarasi kusimamia miradi kwa umakini ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.



Kwa upande mwingine, ameeleza kuwa serikali imetenga fedha katika mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kutatua changamoto za daraja la Ngomalusambwa, daraja la Igagala na barabara za Mchakamchaka, ambazo zimekuwa kero kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.



TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.