Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi- CCM Taifa, Ndg Comrade Mohamed Ali Kawaida, amefanya ziara ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani hapa.
Miradi iliyotembelewa na Comrade Kawaida aliyeambatana na Uongozi wa CCM Mkoa, Wilaya na Kata ya Kasekese, alitembelea ujenzi wa Barabara ya kiwango cha Lami kutoka Kagwila, Karema-Ikola yenye urefu wa 130km, kwa gharama ya Shilingi Bilioni 112.
Pia alipata fursa ya kutembelea mradi wa vijana wa ghala la kutunza na kuuza mazao, pamoja na mashine ya kukobolea mpunga, amapo kikundi hicho kilipatiwa mkopo wa 10% wa mapato ya ndani wenye thamani ya Shilingi Milioni 61 kutoka Halmashauri.
“Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameniagiza nikifika Katavi,nifike hapa Kasekese kwa mambo mawili, moja kuwapa salam zake, na pili kuangalia utekelezaji wa mradi huu wa Barabara ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa alipofanya ziara mkoani humu, nimeridhishwa na kasi ya ujenzi” Comrade Kawaida.
“Niwapongeze Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa kuendelea kutoa mikopo ya 10% kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Nimeambiwa hapa kikundi hiki kimepatiwa Mil 61, sio rahisi kwa sababu nimetembelea Halmashauri nyingine nimekuta wanapewa Milion moja au mbili, kwa pesa hiyo unafanya biashara gani?”
Ziara hiyo ni ya siku moja ambapo imehitimishwa kwa Mwenyekiti wa UVCCM kuzungumza na vijana pamoja na wananchi wa Kata ya Kasekese na Wilaya ya Tanganyika kwa ujumla, na kuwaeleza mambo makubwa yanayofanya na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkr Samia Suluhu Hassan.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.