Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA Wilayani Tanganyika wametakiwa kuhakikisha wanajenga miradi ya barabara kwa kuzingatia ubora na ukamilishwaji kwa wakati wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa wilayani humo.
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Onesmo Buswelu alipokuwa akizungumza na wananchi mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilomita 4 katika kijiji cha Majalila.
“Nikuombe Mkandarasi na Meneja wa Tarura, hakikishe mradi huu unakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia ubora unaotakiwa ili thamani ya fedha hii iweze kuonekana” amesema DC Buswelu,
Mradi huo unaojengwa kwa gharama za kiasi cha shilingi Bilioni 4 unatekelezwa na Mkandarasi Gladiator Investment Limited unatarajiwa kusaidia kuondoa changamoto ya barabara kwa wakazi wa vitongoji kadhaa vya kijiji cha Majalila,
Kwa upande wake Meneja wa Tarura wilaya ya Tanganyika Mhandisi Nolasco Kamasho amesema kuwa, mradi huo utakamilika kwa wakati na ubora utazingatiwa ili thamani ya fedha iliyotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iweze kuonekana,
Mheshimiwa Buswelu alimalizia ziara yake kwa kutembelea mradi wa shule ya sekondari ya Kamsenga katika kijiji cha Katobo wenye thamani ya shilingi Milioni 603 na kuwaagiza mafundi wanaojenga mradi huo kuongeza wafanyakazi na kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi uweze kukamilika kwa haraka na wanafunzi waanze kusomea shuleni hapo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.