Leo Februari 13, katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, kwa Pamoja limeridhia na kupitisha Bajeti ya Shilingi Bilioni 39,250.472,118.00 kwa mwaka wa fedha 2025/26.
Aidha katika bajeti hiyo iliyoainisha makundi ya mchangunuo ya vyanzo vya mapato, imebainisha kwamba:
Mapato ya ndani kwa matumizi ya kawaida ni Tshs Bilioni 4.13
Mapato ya ndani kwa miradi ya Maendeleo Tsh Bil 6.19
Ruzuku ya Serikali Kuu Matumizi ya kawaida ni Tsh Bil 1.38
Ruzuku ya Serikali kuu miradi ya Maendeleo ni Tsh Bil 9.11
Aidha malipo ya mishahara ni Tsh Bil 18.420
Bajeti ya mwaka 2025/26 imejikita katika utatuzi wa changamoto ya miundombinu ya shule za msingi na Sekondari, sekta ya afya, pia vipaumbele vyote ikiwemo mikopo ya 10% kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Sekta ya Kilimo, mifugo na uvuvi ni miongoni mwa vipaumbele vya bajeti hii.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.