Mfuko wa jimbo kuboresha sekta ya Elimu, Afya na Maji wilayani Tanganyika
Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini wilayani Tanganyika Mhe. Moshi Kakoso ameahidi kuendelea kusaidia wananchi wa jimboni kwake kwa kujikita katika vipa umbele vitatu kwanza. Kakoso ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda lililofanyika Oktoba 12, 2017 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda.
“Kila kijiji cha wilaya ya Tanganyika nimehamasisha na kuchangia fedha za kuanzisha mfuko wa maji. Na lengo la kuwa na mfuko wa maji wenye hela katika vijiji vyetu ni kuwa tayari kwa kupokea miradi ya maji kipindi itakapotokea”. Alisema Mhe.Kakoso
Naye mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji mhe.Frank Kibigas “amesema, Katika shule zote 52 zilizotembelewa hali ya utoaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi hairidhishi,Uhamasishaji umefanywa mwitikio unaridhisha isipokuwa kwa baadhi ya maeneo hali bado hairidhishi kama wazazi na walezi walivyoahidi wakati wa kupanga suala hili.
Hata hivyo bado hali ya utoro katika shule za msingi katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ni mkubwa, Serikali za Vijiji ndio wanaotakiwa kuwachukilia hatua wazazi wa watoto watoro lakini hawafanyi hivyo wanapopelekewa majina na walimu Wakuu. Hali hii imejenga usugu kwa suala hili. Aidha swala hili kwa sasa ni changamoto kubwa na linahitaji utatuzi wa kina. Idara imependekeza kuwa iwe agenda ya kudumu kwenye vikao vya maendeleo vya vijiji na kata ambapo wenyeviti wa maeneo husika watawakilisha taarifa za utekelezaji
Kwa kuwa lengo kuu la madiwani ni kuhamasisha maendeleo ya wananchi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John aliwapongeza waheshimiwa madiwani kwa kuwa na moyo wa uzalendo wa kuhamasisha wananchi kujitolea katika kuchangia na kutekeleza shughuli za kimaendeleo. Hadi sasa viongozi kwa kushirikiana na wananchi wamejenga vyumba vya madarasa na ofisi za walimu vipatavyo 97
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.