Madiwani wapongeza miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2017.
Na Sylvanus Ntiyakenye
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Mpanda limepongeza ofisi ya Mkurugenzi mtendaji na wataalamu wake kwa kusimamia miradi vizuri. Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mhe. Hamad Mapengo kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika Mei 5, 2017 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda (Idara ya maji).
“Mkurugenzi na wataalam kwa ujumla nawapongezeni kwa kuchapa kazi usiku na mchana na kuhakikisha miradi yote iliyopitiwa na mwenge inakuwa na ubora wa hali ya juu. Sasa tuanze kuelekeza nguvu zile zile zilizotumika katika maandalizi ya mwenge, kwa mwenge ujao (2018)”. Alisema Mhe. Mapengo.
Mwenge wa uhuru 2017 ulikuwa na hamasa kubwa sana kutoka kwa wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Hamasa ilisababishwa na kuwepo kwa kamati shirikishi kati ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Tanganyika, ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda na wananchi.
Kamati ya hamasa ilifanya kazi kubwa na kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwa wingi kuushangilia na kuupokea mwenge wa uhuru katika maeneo yao.Mwenge wa uhuru 2017 uliwashiwa mkoani Katavi Aprili 2, 2017 na kukimbizwa katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda (Tanganyika) Aprili 3, 2017 na kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbali mbali.
Naye diwani wa kata ya Tongwe Mhe.Frenk Kibigas amempongeza mwenyekiti wa kamati ya Elimu , Afya na Maji mhe. Michael Kapata pamoja na Watalaamu wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kusimamila na kukamilisha mradi wenye uwezo wa kuwahudumia watu zaidi ya elfu tatu (3,000). Mradi wa maji wa Majalila una matenki mawili yenye uwezo wa kujazwa lita 180,000 na chanzo cha maji ya kutosha yanayovutwea na umeme jua.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.