Baada ya kupita miaka mingi bila kuwa na shule ya Sekondari hatimaye wananchi wa Kijiji cha Bujombe wamshukuru Mhe Rais Samia Suluhu kuwapatia fedha za ujenzi wa shule itakayowaondolea adha wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kwenda Mwese kwaajili ya masomo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe Onesmo Buswelu amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa katika Kata ya Katuma na Mwese, ambapo katika Kijiji cha Bujombe ameweka jiwe la msingi ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, vyoo pamoja na jengo la ofisi za walimu.
Katika uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa shule ya Sekondari Mh Buswelu amewataka wananchi kuendelea kuhifadhi misitu kwa faida za maendeleo mengi kwa kizazi cha sasa na baadae, huku akisisitiza kasi kubwa kuongeza ili kukamilisha ujenzi wa mradi huo.
Kupitia ziara hiyo DC Buswelu ametoa maagizo SITA ikiwemo usajili wa shule shikizi ya mlimani kuanza mara moja, urejeshaji wa maji katika shule ya msingi shikizi ya mlimani, kupeleka maji kwaajili ya kuogeshea mifugo katika josho la Kapanga, kutunza misitu, kuwataka wananchi kushiriki kwenye uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu, pamoja na kuwataka wakandarasi na mafundi wote wenye miradi kuwa eneo la kazi na kukamilisha kazi kwa wakati.
Aidha wakazi mbalimbali wa Kijiji cha Bujombe ikiwemo fundi ujenzi wa mradi huo, wameupokea vizuri mradi huo na kuahidi kuanzisha benki ya matofali ya kuchoma kwaajili ya ujenzi wa miradi mingine shuleni hapo.
Pia mradi huu umepokea kiasi cha shilingi milioni 144, ambayo ni mapato yanayotokana na biashara ya kaboni Wilayani tanganyika, ambapo Kijiji hicho kimeingiziwa shilingi Bilioni 1.34 ya mapato yote ya biashara hiyo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.