SATF YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 300 HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA, YAAHIDI KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DKT. SAMIA KUBORESHA ELIMU NCHINI.
Katika jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Taasisi isiyo ya kiserikali ya Social Action Trust Fund (SATF) leo imekabidhi msaada wa Madawati 300 yenye thamani ya Shilingi Milioni 15,000,000 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika hapa Mkoani Katavi,
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Madawati hayo iliyofanyika katika viunga vya Shule ya Msingi Kasekese, Mratibu wa SATF Bi. Helena Chikomo amesema kuwa wanayo furaha kuona na wao wanasaidia kuhakikisha mtoto wa kitanzania anapata elimu yake akiwa katika mazingira bora na salama kwa kusaidia mahitaji mbalimbali ya elimu kama madawati, madaftari, taulo za kike na vifaa vingine,
Bi. Helena aliongeza kwa kuwataka wanafunzi wa Shule ya Msingi Kasekese kuhakikisha wanayatumia vizuri madawati hayo kwa kuyatunza ili yaweze kudumu na kutumika na kizazi cha sasa na kile cha baadae,
Aidha, Kaimu Afisa Elimu Msingi Wilayani Tanganyika Bw. Ojung Sabaya aliwashukuru SATF kwa msaada wao wa madawati 300 na kuwaomba kuendelea kuwashika mkono kadri watakavyoona inafaa ili kwa pamoja waweze kuhakikisha watoto wilayani Tanganyika wanapata elimu katika mazingira yaliyo bora,
Mwisho, Kaimu Afisa Elimu Msingi Bw. Ojung Sabaya aliwataka Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi Kasekese kutumia vizuri Madawati hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu na kusaidia vizazi vingi vinavyokuja.
@social_action_trust_fund @ortamisemi @samia_suluhu_hassan @wizara_elimutanzania @mkoa_katavi
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.