• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Tanganyika District Council
Tanganyika District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanganyika District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

ALAT KataviI yapongeza miradi ya Halmashauri ya wilaya ya Mpanda

Posted on: May 24th, 2017

Wajumbe wa ALAT tawi la mkoa wa Katavi wamepongeza Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kuwa na mradi wa maji mkubwa na unaotumia umeme jua. Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa ALAT wa mkoa wa Katavi Mstahiki Meya William Mbogo.

“Nawapongeza watalaam pamoja na ofisi ya Mkurugenzi kwa kuwa na mradi unaotumia umeme jua.  Halmashauri zingine tujifunze kuwa na miradi ya maji inayotumia umeme jua kama wenzetu wa Mpanda DC walivyofanya….” 

Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Majalila umegharimu shilingi 703,501,240 hadi kukamilika kwake. Mradi umetekelezwa katika awamu mbili. Awamu ya kwanza ilikuwa ujenzi wa matenki mawili yenye ujazo wa lita 180,000 na ufungaji mabomba ya maji ‘civil works and pipe fitting’. Hata hivyo awamu ya pili ilijikita katika ufungaji wa umeme jua, utengenezaji wa ua na pampu ya kuvuta maji.

Wakazi wa kijiji cha Majalila ambapo ndipo panapojengwa makao Makuu ya halmashauri ya wilaya ya Mpanda wananufaika na mradi huo kwa kupata maji safi na salama.

Hata hivyo, kamati ya ALAT tawi la Katavi iliendelea na ukaguzi wa miradi iliyopitiwa na mwenge wa Uhuru 2017 katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Miradi hiyo ni pamoja na jengo la utawala la shule ya sekondari Mpandandogo uliogharimu shilingi 64,680,396.40.

Miradi mingine ni vyumba sita vya madarasa na ofisi moja katika shule ya msingi Kasekese. Halmashauri ya wilaya ya Mpanda imeshirikiana bega kwa bega  na wananchi wa Kasekese kuhakikisha kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa.

“Mheshimiwa mwenyekiti, shule ya msingi Kasekese ina zaidi ya wanafunzi 1,600 na robo tatu yao walikuwa wanasomea nje. Kukamilika kwa ujenzi wa vyumba sita vimesaidia sana kuongeza hamasa ya wanafunzi ya kupenda shule….” Alisema Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw.Romuli John.

Hata hivyo kamati ya ALAT iliendelea na ukaguzi wa mradi wa zahanati ya kijiji cha  Itetemya unaotekelezwa kwa ufadhili wa serikali kuu kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF III kwa kushirikiana halmashauri ya wilaya ya Mpanda pamoja na wananchi wa kijiji hicho. Mradi huo umegharimu shilingi 76,391,800.  Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya kuishi walimu sita, vyumba vitatu vya madarasa na matundu matano ya vyoo vilivyojengwa katika shule ya sekondari ya Ikola.

Baada ya wajumbe kutembelea miradi iliyopitiwa na mwenge, walihitimisha kwa kufanya kikao cha majumlisho. Kikao hicho kilifanyikia katika ukumbi wa mwolo wa Ikola katika kijiji cha Ikola. Kikao kilimuidhinisha Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John kuwa katibu wa ALAT tawi la Katavi kushika nafasi ya aliyekuwa katibu wa ALAT Bw. Ngalinda Ahmada aliyefariki Dunia Disemba 01, 2016.

Wajumbe walikubaliana kwa pamoja kuwa fundi wa kawaidi (local fundi) anapojenga mradi katika halmashauri zilizopo mkoani Katavi asilipwe fedha nyingi. Inatakiwa alipwe kutokana na kazi aliyofanya na siyo kumpatia hela nyingi ambazo haziendani na alichofanya katika mradi. Mafundi wengi wamekuwa wanachelewesha kazi kwa kuwa wao ndio wanaodaiwa kukamilisha kazi.

                                                                                                                                                                                                               

 

Matangazo

  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA May 27, 2025
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA DEREVA II, KATIBU MAHSUSI III NA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UKUSANYAJI WA KODI WAPAA TANGANYIKA – DC: 'NDIYO NJIA PEKEE YA KULETA MAENDELEO'

    May 27, 2025
  • UKUSANYAJI WA KODI WAPAA TANGANYIKA – DC: 'NDIYO NJIA PEKEE YA KULETA MAENDELEO'

    May 27, 2025
  • HALMASHAURI ZA WILAYA YA MOMBA NA MAKETE ZAKUTANA WILAYANI TANGANYIKA KUJIFUNZA BIASHARA YA KABONI.

    May 26, 2025
  • TANGANYIKA KUENDELEA KUWEKA MIKAKATI KUBORESHA SUALA LA LISHE, WAKUU WA IDARA YA ELIMU NA WAKUU WA SHULE WAPEWA MBINU KUSIMAMIA UPATIKANAJI CHAKULA MASHULENI.

    May 13, 2025
  • Tazama zote

video

MILIONI 328 KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA TFS TANGANYIKA, DC BUSWELU ASISITIZA UBORA WA MAJENGO.
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA TANGANYIKA
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    TONGWE - MAJALILA

    Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA

    Telephone: +255-252955264

    Simu ya mkononi: 0754870344

    Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.