• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Tanganyika District Council
Tanganyika District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanganyika District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

UKUSANYAJI WA KODI WAPAA TANGANYIKA – DC: 'NDIYO NJIA PEKEE YA KULETA MAENDELEO'

Posted on: May 27th, 2025

 

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Wilaya ya Tanganyika imefanikiwa kukusanya mapato yaliyovuka lengo kwa zaidi ya asilimia 100 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kuanzia Oktoba 2024 hadi Aprili 2025. Hayo yameelezwa katika kikao rasmi kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, ambaye ni Mwenyekiti wa kikao, amepongeza mafanikio hayo na kuongeza kuwa ni hatua muhimu kuelekea maendeleo ya wananchi.

Akizungumza katika kikao hicho, DC Buswelu ameeleza kuwa mafanikio ya ukusanyaji huo wa mapato ni kielelezo cha uwajibikaji na ushirikiano mzuri kati ya serikali na wananchi. Amesema, "Ukusanyaji huu unaleta taswira ya chachu ya maendeleo kwa wananchi wetu, kwani mapato haya ndiyo yanayowezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi."

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Hamad Mapengo, amepongeza TRA kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato na kuwahimiza waendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ulipaji wa kodi bila usumbufu. "Wananchi wakielimishwa vizuri, wataelewa wajibu wao na kuchangia kwa hiari maendeleo ya taifa letu," amesema Mapengo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tanganyika, Juma Shaban Juma, amesifu mafanikio hayo na kuwataka TRA kuendeleza ushirikiano uliopo kati yao na viongozi wa serikali, akieleza kuwa ushirikiano huo ndio msingi wa mafanikio endelevu katika ukusanyaji wa mapato.

Naye Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tanganyika, Said Wambari, ametoa wito kwa wananchi kulipa kodi kwa hiari bila kushurutishwa, akibainisha kuwa ni kwa njia hiyo tu serikali itaweza kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake Katibu wa kikao ambaye pia ni Meneja Msaidizi wa TRA Mkoa wa Katavi Bernard Peter, ameeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na mikakati madhubuti ya uhamasishaji, usimamizi na ushirikiano mzuri na wadau mbalimbali. “Tumefanikisha ukusanyaji wa mapato kwa zaidi ya asilimia mia moja, jambo linaloonyesha utayari wa wananchi kushiriki katika maendeleo ya nchi yao,” amesema Bernard.

Matangazo

  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA May 27, 2025
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA DEREVA II, KATIBU MAHSUSI III NA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UKUSANYAJI WA KODI WAPAA TANGANYIKA – DC: 'NDIYO NJIA PEKEE YA KULETA MAENDELEO'

    May 27, 2025
  • UKUSANYAJI WA KODI WAPAA TANGANYIKA – DC: 'NDIYO NJIA PEKEE YA KULETA MAENDELEO'

    May 27, 2025
  • HALMASHAURI ZA WILAYA YA MOMBA NA MAKETE ZAKUTANA WILAYANI TANGANYIKA KUJIFUNZA BIASHARA YA KABONI.

    May 26, 2025
  • TANGANYIKA KUENDELEA KUWEKA MIKAKATI KUBORESHA SUALA LA LISHE, WAKUU WA IDARA YA ELIMU NA WAKUU WA SHULE WAPEWA MBINU KUSIMAMIA UPATIKANAJI CHAKULA MASHULENI.

    May 13, 2025
  • Tazama zote

video

MILIONI 328 KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA TFS TANGANYIKA, DC BUSWELU ASISITIZA UBORA WA MAJENGO.
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA TANGANYIKA
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    TONGWE - MAJALILA

    Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA

    Telephone: +255-252955264

    Simu ya mkononi: 0754870344

    Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.